Hot Posts

6/recent/ticker-posts

LEO NI TBT ||YANGA Jana imeshinda Magoli 5-0

 LEO NI TBT ||YANGA Jana imeshinda Magoli 5-0


dhidi ya kmc na imewachukua miaka kumi tokea wameshinda ushindi mkubwa Ivo kwenye ligi na ilikuwa dhidi ya Ashanti united walishinda goli 5-1 vs Ashanti united msimu wa 2013/2014 


Wakati yanga anapiga mtu Kono la nyani Tano Moja  dhidi ya Ashanti ilikuwa pia ni mechi ya kwanza kwenye ligi kama ilivo Jana dhidi ya kmc wakati huo Simba nao waliocheza mechi Yao ya kwanza dhidi ya Rhino rangers na kutoka Sara ya 2-2


Mabao ya Yanga kipindi icho yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya 90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89.


KIKOSI CHA YOUNG AFRICANS (YANGA) KWA MSIMU 2013-14 


Makipa | Ali Mustafa, Deo Munishi na Yusuph Abdul. Beki Kulia | Mbuyu Twite na Juma Abdul. Beki Kushoto David Luhende na Oscar Joshua Beki Kati | Nadir Haroub, Kelvin Yondani na Rajab Zahir. Viungo | Athuman Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Salum Telela, Reliants Lusajo, Nizar Khalfan. Staika | Didier Kavumbagu, Jerryson Tegete, Mrisho Ngassa, Shaaban Kondo na Hussein Javu. Hichi ndicho kikosi cha wachezaji 22 Yanga kwa  kipindi icho.


@mudathir__yahaya27 Jana baada ya kuwapa somo uwanjani kwenye mechi aliwapa somo pia baada ya mechi wapinzani


Anaandika 🖊️ @alexander_aloyce_minja

Post a Comment

0 Comments