Mwaka 2016 wakati msanii Darassa amesimamisha game nzima ya Bongo Fleva kwa wimbo wake wa Muziki akiwa na Ben Pol, Kila mtu alikubari.
Hakuna sehemu ambayo wimbo haukupigwa, Hakuna Club au popote pale ambapo DJ asingeweza kuupiga ulikuwa wimbo wa Taifa Darassa at his best.
Ni 2016 ikiwa imeambatana na matukio mengi, Ni 2016 Kioo cha Tanzania Mbwana Samatta alijiunga na Genk ya Ubeligiji, Ilikuwa ni safari yake katika harakati za kuitafuta ndoto ya kucheza EPL.
Ni 2016 ambayo haiwezi kusahaulika, Mikono mizito iwapo ulingoni ilipoteza maisha namzungumzia bingwa wa ndondi Thomas Mashali.
Na ni 2016 ambayo Cristiano Ronaldo aliingoza Ureno kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kushinda ubingwa wa Euro mbele ya Ufaransa.
Wakati matukio mengi yakizuka mwaka 2016, Playmaker Mesut Ozil alituonesha maana halisi ya kiungo mshambuliaji mwenye maarifa mkubwa kichwani.
Sikia sasa, Usiku mmoja pale Bulgaria, Arsenal wanapewa goli mbili kupitia kwa Jonathan Cafu na Claudiu Kaseru, Ni Ludogorets dhidi ya Arsenal.
Granit Xhaka na Mfaransa Giroud kwa mabao yao, Arsenal wakarudi mchezo, Wakaanza kutawala kwa zile pasi zao siunajua Arsenal na pasi ni ndoa ya milele, Ozil alifanya nini?
Mtoto kutokea Afrika ya Kaskazini, Namzungumzia Mwarabu Mohamed Elneny katikati ya dimba anauvusha mpira kwenda kwa Mjerumani mwenye asili ya Uturuki, fundi mmoja hivi.
Mesut Ozil akafunga bao la akili kubwa, Bao ambalo kila aliesikia simulizi angetamani kuliona. Huwa hayatokea kirahisi.
Baada ya kuupokea mpira anasogea kulitafuta lango la Ludogorets Razgrad, Goalkeeper Milan Borjan anasogea anapewa kanzu kwa aina ya Lionel Messi.
Walinzi wawili wanawahi kumzuia Mesut Ozil, Ozil anapiga step moja kama anafunga kumbe anadanganya walinzi wote wanalamba nyasi, Ilikuwa ni IQ kubwa ndani ya kichwa cha Ozil.
Alifikiri haraka na mguu ulimtii Ozil, Ulikuwa usiku wenye simulizi nzuri kupitia mguu wa Ozil, Arsenal wakifuzu hatua ya 16 bora ya Klabu bingwa ulaya.
Kama Mesut Ozil angekuwa chini ya wakala maarufu bwana Mino Raiola, Usiku ule Ozil alikuwa na thamani ya Euro million 150. Ozil alifunga bao la mateso pale Bulgaria.
0 Comments