Kocha Robertinho amesema Simba haina presha ya kukutana na timu yoyote msimu huu na kwamba hesabu zake sio tu kutaka kuwang’oa Power Dynamo bali ni kuwafunga kwao kisha kuwamalizia hapa nchini kwenye mchezo wa marudiano
.
“Tuna kikosi imara sana kitu bora ambacho nafurahia ni kubaki kwa msingi wa timu yangu ya msimu uliopita hii ni muhimu sana sasa ukija kuongeza na hawa wapya sina wasiwasi na timu yoyote kwasasa,” alisema Robertinho na kuongeza
.
“Tunawaheshimu Power Dynamo ni timu nzuri, nadhani kila mmoja anakumbuka walivyocheza na sisi hapa kwenye siku ya Simba, lakini Simba ni klabu kubwa Afrika tunajipanga kuanza na hesabu za kushinda
kuanzia ugenini ili tumalizie mchezo hapa nyumbani.”
.
Alisema katika kujiweka fiti ndio maana ameomba mechi za kirafiki kabla ya kuanza mechi za Ligi ya Mabingwa.
0 Comments