Hii ndio Ligi kuu ya soka nchini England . Just imagine being us ... just imagine it . Pungufu uwanjani tangu dakika ya 28 lakini Liverpool wamecheza kama wapo 15 uwanjani
1: Nidhamu ya mchezo
2: Kujipanga vizuri uwanjani
3: Ufundi
4: Matamanio ya kupambana
5: Passing
6: Hakuna mvivu uwanjani
7: Ukatili mbele ya goli
This is Liverpool brother and sisters
✍🏻Kipindi cha kwanza unaangalia hii mechi ina kila kitu unachotaka kutoka kwa team ambazo zipo serious na kazi zao . Pressing ya hali ya juu, pasi za umakini sana , kuwania mpira , kasi ya mchezo na wachezaji wenyewe .
✍🏻Baada ya kadi nyekundu kwangu mimi hapo ndio mechi ilianza rasmi kwa timu zote mbili kivipi ?
✍🏻Klopp akaihamisha timu yake kuwa 4-4-1 bila mpira ( Salah pekee mbele ) huku mstari wa wachezaji wanne kati Elliot Szobo Jota Mac Allister kabla ya Darwin kuingia dimbani lakini bado muudo ukawa ule ule ulibadilika wakiwa na mpira tu
✍🏻Wakiwa na mali Liverpool wanakuwa 2-4-3 ( nyuma Jarell na Gomez ) then TAA , Elliot Szobo na Robbo na mbele Jota Salah na Darwin
✍🏻Newcastle walijipiga risasi mguuni
1: Walianza kucheza na hisia sana badala ya kutumia akili na utulivu na hiyo kutokana na mashabiki wao
2: Wakaanza kulazimisha kwenda mbele haraka kwa pasi nyingi za kwenda mbele badala ya kumiliki mpira na kuwafanya Liverpool wautafute
3: Pembeni ndio ilikuwa suluhisho zuri kwao ili kuwafanya Liverpool kuzuia eneo kubwa la uwanja kwa kuwatumia Almiron na Barnes badala yake waliendelea kulazimisha kupita katikati.
4: Unawapa pongezi kubwa Liverpool kwa uzuiaji wao licha ya kuwa pungufu .
NOTE:
1: Mechi ya pili Liverpool wanacheza pungufu na bado wanashinda mechi 🔥
2: TAA kosa la pili mfululizo la TAA na anaadhibiwa
3: Gordon leo alimpika sana TAA 🔥
4: Sidhani kama kunatakiwa kuwe na mjadala kuhusu ALISSON BECKER . kipa bora Duniani full stop 🔥
5: DARWIN NUNEZ nafasi mbili kamba mbili : Clinical , ruthless, lethal 🔥🔥
6: KAMA NEWCASTLE WAMEONEWA LETA TIMU YAKO TENA LIVERPOOL WAKIWA PUNGUFU
FT: Newcastle 1-2 Liverpool
0 Comments