Siku moja baada ya timu ya Simba kurudi kambini na kuanza mazoezi, Kocha Mkuu, Robertinho amesema siku 30 za mapumziko zinahitaji mechi za kirafiki ili kuweka kikosi chake kwenye ushindani.
.
“Timu imecheza mechi mbili na kupata mapumziko nahitaji kuwa na mazoezi mepesi na ya nguvu, lengo ni kuitengeneza timu ya ushindani ndani ya dakika zote 90 haitakuwa rahisi kama tutafanya mazoezi bila mechi za kirafiki;“
.
“Nimeongea na viongozi kuhakikisha wananitafutia timu ambazo zitawapa changamoto wachezaji lengo ni kujenga utimamu na kuwapa pumzi kwani tuna mashindano mengi mbele.” alisema Robertinho.
.
“Nina kazi kubwa ya kufanya kuijenga timu ya ushindani na iliyo na pumzi ya kucheza dakika tisini bila kuwa na mabadiliko. Hivyo mechi za kirafiki na mazoezi ya mara kwa mara yatanifanya nijenge timu shindani na bora kazi ya viongozi imeisha sasa ni jukumu langu kutengeneza kikosi imara na bora.”
0 Comments