Hot Posts

6/recent/ticker-posts

YANGA VS JKT TANZANIA KOCHA GAMONDI ATAMBA KIBABE


"Nina heshimu kila mpinzani ambaye tunakutana nae, falsafa yangu ni kucheza mchezo mzuri bila kujali tunacheza na nani, lengo letu kubwa ni matokeo pamoja na furaha kwa wananchi".

Miguel Gamondi kocha mkuu wa klabu ya Yanga

 “Mimi sipendelei kusema mchezaji yupi atakuwepo au yupi hatakuwepo, kikubwa hali za wachezaji wetu zipo sawa, tumekuwa na ratiba ngumu kidogo baada ya kucheza mechi 3 ndani ya siku 10, tena kwenye viwanja vya nyasi bandia, viwanja vya nyasi bandia sio vizuri sana husababisha majeraha kwa wachezaji lakini uzuri ni kwamba wachezaji wetu wote wapo salama".


Miguel Gamondi kocha mkuu wa klabu ya Yanga 🔰
"Kuna wachezaji kadhaa waliokumbwa na majeraha mchezo uliopita lakini kwa sasa wapo salama na tayari kuwavaa wapinzani wetu siku ya kesho na kuhusu Skudu ameshaanza mazoezi ya gym jana na wiki hii tutamweka kwenye uangalizi kisha baada ya hapo ataanza mazoezi na wachezaji wenzake".

Miguel Gamondi kocha mkuu wa klabu ya Yanga 🔰
“Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi, ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyuma nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi".

Miguel Gamondi kocha mkuu wa klabu ya Yanga 🔰

Post a Comment

0 Comments