.
Neville amemwambia Arteta atulize akili yake wakati atakapomenyana na kocha Erik ten Hag na jeshi lake la Man United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa Jumapili.
.
“Ninachoweza kusema, ukiitazama Arsenal ni kama kuna majaribio hivi,” alisema mchambuzi huyo wa Sky Sports. “Mabeki wa pembeni wanachezeshwa kwenye kiungo na viungo wanachezeshwa kwenye nafasi ya mabeki wa pembeni.”
.
“Thomas Partey hatumiki vyema kwenye mechi. Wakati mwingine unahitaji kurudi kwenye misingi halisi. Namtarajia Mikel Arteta ataacha majaribio yake wiki hii na kurudi kwenye ile safu yake kamili ya mabao.”Na Neville aliongeza kwamba ile nafasi anayocheza Partey kwa sasa inapaswa itazamwe upya na majaribio hayo yasiendelee kwenye mechi dhidi ya Man United kama kweli Arsenal wanahitaji kupata ushindi katika mchezo huo.
.
“Partey arudishwe kwenye kiungo akacheze na Declan Rice na Martin Odegaard,” alisema Neville na kuongeza. “Arudishe na apange timu vile ambavyo inapaswa kuwa.” Arsenal imekuwa ikipewa nafasi ya kuwa mshindani wa Man City kwa mara nyingine kwenye mbio za ubingwa msimu huu baada ya matumizi makubwa kwenye usajili wa dirisha hili.
0 Comments