“Familia ya Bakhresa kupitia kwa Abubakar Bakhresa imewaahidi wachezaji wake donge nono endapo watashinda mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Bahir Dar na kufuzu hatua inayofuata.”
“Wakishinda leo tutatoa taarifa rasmi kupitia mitandao ya klabu kuwa wamepata kiasi gani, lakini kuna mzigo umeandaliwa kwa ajili ya timu nzima.”
“Kuna mzigo mwingine mkubwa zaidi kama tutavuka hatua inayofuata kwa kuitoa Club Africain na kwenda hatua makundi.”
- Hasheem Ibwe, Ofisa Habari Azam FC.
“Timu yetu inasukwa upya, Youssouph Dabo tangu ameingia na benchi lake jipya la ufundi, anachokifanya ni kuanza kuingiza falsafa na mbinu zake ili timu icheze anavyotaka yeye.”
“Anatamani kuona timu inakaba zaidi lakini vilevile inacheza soka la kasi zaidi. Sisi tunamuunga mkono licha ya kwamba tumepoteza baadhi ya michezo muhimu kwenye Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho.”
“Bado tuna timu nzuri na tunaamini tunaweza kufuzu kutoka hatua ya awali kwenda hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho la CAF.”
- Hasheem Ibwe, Ofisa Habari Azam FC.
0 Comments