“Jumapili iliyopita tulicheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asas Djibouti FC kikanuni tulikuwa ugenini, Jumamosi hii tutacheza mchezo wa marudiano tukiwa wenyeji.”
“Tukishinda mechi hiyo tutakuwa tumevuka hatua ya awali kwenda hatua inayofuata ambayo itakuwa imetutenganisha na hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”
“Tuna zaidi ya miaka 20 hatujacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika! Kila mwanachama, kila shabiki na mpenzi wa Yanga anasubiri kwa hamu kuiona timu yetu inacheza hatua ya makundi.”
“Tulishakuwa wazi kwa mashabiki mapema kabisa kwamba, lengo letu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu ni kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”
“Kwa hiyo nawakaribisha mashabiki wa Yanga kwa wiki uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 11:00 jioni.”
- Ally Kamwe, Mkuu wa Habari na Mawasiliano Yanga.
0 Comments