Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SOMO LA SHAFFIH DAUDA👊👊👊✍️✍️

 

Unaitazamaje dunia? Unaamini una uwezo watu wanakubania? Jibu lipo suluhisho ni Teknolojia, unatumiaje Instagram, Twitter, Tiktok na Facebook yako? Ifanye kuwa ofisi yako na onesha uwezo wako. 


Kama ni Mwalimu fungua Youtube ama mtandao wowote piga lecture watakuona tu, rejea Joyce Kiango kutoka Dodoma mpaka Azam TV, kama ni Daktari fungua akaunti tupe hints kuhusu afya watakuona tu watakufuata, kama ni Mhandisi fungua akaunti tupe hints kuhusu sekta yenu, watakuona tu. 


Taratibu dunia imehama kwenye kutangaza ajira na kusambaziana CV bali kumtafuta anayeonesha na kumpa nafasi, leo hii Khaby Lame ni Bilionea kupitia Instagram, kuna Mtoto Brazil ni Bilionea kupitia Instagram, taratibu dunia inatupa maana ya nguvu ya social media.


Unafungua social networks kutukana ama kulalamika, wenzako wanafungua na lengo na kutoka kwenye ufukara, serikali haiwezi kuajiri wakati wote, taasisi haziwezi kuajiri wakati wote ila wape sababu ama jipe sababu ya kupata ajira, unayo nafasi. 


DIGALA anatamani kuona kizazi cha fikra nje ya box, keki hii ni kubwa sana unayo nafasi yako! Be a solution to every problem and not a problem to every solution. 


WHEN DIGALA SPEAKS, YOU LISTEN.

Post a Comment

0 Comments