Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TFF YAOMBA MSAMAHA CAF KISA TAMKO LA WAZIRI DAMAS NDUMBARO

 


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeandika barua kwenda kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf ) likiomba msamaha na kueleza kuwa mechi zitachezwa kwa kufuata kanuni na taratibu za soka na hakutakuwa na zuio lolote kwa mashabiki. 

.

Hii ni baada ya kauli iliyotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro, ili shabiki wa timu pinzani ya Simba au Yanga aruhusiwe kuingia uwanjani katika mechi hizo za mwishoni mwa wiki ijayo, anapaswa kuonyesha hati yake ya kusafiria ya nchi inazotoka timu hizo akilenga kuhamasisha uzalendo, japo alishaanza kupingwa na baadhi ya wadau mapema.

.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalihakikishia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mechi husika itachezwa kwa kanuni na taratibu zilizowekwa za soka na namna ya utaratibu wa kuingia uwanjani.“

.

“Kwa hivyo, sio kwamba pasipoti (pasi za kusafiria) zitatumika kama kigezo cha kuingia uwanjani kwa mashabiki wa Mamelodi Sundowns na mtu yeyote kwa sababu mechi ipo kikanuni na taratibu za mpira wa miguu bali sio kwa Idara ya Uhamiaji.“

.

Timu ya Mamelodi Sundowns imehakikishiwa usalama wao kutoka kwa vyombo husika wakati wote ambao watakuwa nchini na kuheshimu taratibu za mechi yao dhidi ya Young Africans SC, na Dhamana hii pia inawahusu maafisa wa mechi, mashabiki wa Sundowns wanaosafiri pamoja na mashabiki wanaoishi Tanzania 

na anaetaka kuhudhuria mechi hiyo,” ilifafanua barua hiyo ya TFF.

Post a Comment

0 Comments