Hot Posts

6/recent/ticker-posts

NICKSON KIBABAGE NDANI YA YANGA ANAENDELEA KUPATA EXPOUSURE YA KUTOSHA

 


NICKSON KIBABAGE kwenye umri wake mdogo anacheza mechi kubwa dhidi ya watu wenye sifa ya physique kama Medeama na mfumo mgumu wa 3-5-2 ambao Yanga walikuwa wanapoteza mipira mara kadhaa na bado amekupa mechi nzuri sana. 


Nilipoandika jana kuwa Marcelo wa Milima ya Uluguru ameupiga sana wala sikuwa naota ama namtetea kwakuwa ni Homeboy, nawapa homework nendeni kwenye sites za ratings anzeni na Sofascore, mchukue Nick na beki wa kushoto wa Medeama yule Kamaradini Mamudu, Nick kamzidi yule beki wao wa kushoto kwa ratings 6.5 kwa 6.4 tena wale walikuwa wanacheza 4-3-3. 


Achana na hiyo chukua Mabeki watano wa Yanga na Mabeki wanne wa Medeama jumla ni Mabeki TISA kwenye mechi ya jana, Beki aliyeperform kwenye kiwango cha juu zaidi ana ratings ya 7.3 nae ni Yao Yao akifuatiwa na Ibrahim Bacca kisha Nickson Kibabage akitokea pembeni. 


Ukichukua Mabeki wote TISA, Nickson ni Beki wanne aliyeperform zaidi kwenye mechi ya jana, maana yake ukichanganya timu zote mbili bado anapata namba, haikuwa mechi rahisi jana kwa Mabeki ila alicheza mpira wa maana sana, hatuwezi kukubaliana kirahisi hapa kwakuwa Nickson ana passport ya Jamhuri, kazaliwa Morogoro na ana ndui bega la kulia, MEN LIE, WOMEN LIE BUT NUMBERS DONT LIE. 


Kabla ya kuja kubishana nendeni kwanza mkajiridhishe kwenye takwimu, tunahitaji FACTS sio OPINIONS, tusiweke maoni tuje na DATA, maoni hata Mwanangu Riyad anaweza akaweka tu😀! Yanga hajacheza na Winga jana, huyu Mtalaam ndio alikuwa anatembea na chaki zote, hiyo ni energy to and flow, aliruka na Kwado yule right back wao ndio Mchezaji hatari zaidi ila Nick alicheza nae.


Leo ni 9 DESEMBA, ni kumbukizi ya Uhuru wa Tanganyika, nao uendane na uhuru wa kifikra na tujitoe kwenye nyororo za kuwaamini Wageni zaidi hata wakifanya vitu vya kawaida uwanjani. 


VISIT MOROGORO🇹🇿

Post a Comment

0 Comments