Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA WAKWAMA KWA NABI, SVEN NA BENTCHIKA, YATUA UFARANSA



Simba SC wamekwama Kwa makocha watatu waliokuwa wanawawania ili kuja kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Robertinho aliyetimuliwa hivi karibuni.


Taarifa za uhakika ni kuwa makocha wote watatu wamekataa ofa ya kuifundisha timu hiyo Kwa sababu tofauti. Nabi ilikuwa ngumu kumpata sababu ndio kwanza ameanza kuisuka AS FAR Rabat ambapo Kwa pesa anayopewa na pia waajiri wake wasingekubali aondoke. Pia Nabi hakutaka kuharibu mahusiano mazuri na mashabiki wa Yanga.


Sven Vandenbroeck yeye aligoma tangu mwanzo kujiunga na waajiri wake wa zamani na akasema anatamani kufundisha Afrika Kusini ambapo anahusishwa na kujiunga na Kaizer Chiefs iliyo katika mazungumzo ya mwisho na kocha huyo.


Kuhusu Bentchika kilichoshindikana ni maslahi binafsi ambapo chanzo Cha kuaminika kinasema ofa ya kocha huyo ni kubwa mno na gharama hizo hawazimudu hivyo mazungumzo kufika njiani kwani kocha huyo wa zamani wa USM Alger aligoma kushusha ofa yake.


Kwa Sasa inasemekana Simba wanehamishia nguvu zao Kwa kocha Fernando Da Cruz raia wa Ufaransa ili kuja kuwanoa wekundu hao japo Kuna upinzani mkubwa kwani kocha huyo anawaniwa pia na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.


Fernando Da Cruz amewahi kuwa kocha mkuu wa AS FAR Rabat ya nchini Morocco.

Post a Comment

0 Comments