Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MSHERY UENDA NI MZURI KWA YANGA KULIKO METACHA HII NI KLABU BINGWA BHANA

 


Wakati wa fainali pale Algeria ya Shirikisho tukiwa na Kocha Nabi baada ya Press Conference nilimuuliza swali off mic kuhusu Magolikipa ambao ni Sweepers akaniambia silaha muhimu moja wapo kwa Yanga ni aina hii ya Makipa (Diarra na Mshery) kwenye build up mstari wa chini wa Yanga ni watu watano yani hesabu Mabeki wanne na Kipa wao, wote wanacheza. 


Kwenye escape plan Mabeki wote wapo huru kugeuka na kuanza na Kipa, tazama mechi za Diarra ama Mshery wanatoka wanasaka space wanapewa pass wanaanzisha mashambulizi na hiyo imekuwa kama mtego mgumu sana kwa Wapinzani, hata jana nilipoona kikosi nikasema Mshery alipaswa kuanza mbele ya Metacha. 


Kama unabisha rejea mechi kwa utulivu kuna matukio zaidi ya manne ya Joyce Lomalisa yupo wakati mgumu ana mpira na Waarabu wanampress ila akigeuka Kipa hajafungua na haoneshi kuitaka mali, analazimika kuforce mbele! Watazame Mabeki wa kati na Yao Yao wakipata mali ilikuwa lazima waforce ipande kwakuwa wanakosa Nyanda wa aina za kucheza. 


Metacha sio Kipa mbaya, wala Yanga haijafungwa kisa yeye ila mfumo wao Wananchi kwasasa unamtaka Sweeper langoni kwa msimu wa tatu na nusu sasa wanaelekea, ijapo Kocha ndie mjuzi zaidi. 


Ubaya hatukupingana kwa hoja! Watu wakaanza Yanga sio ya Morogoro, mara kisa Mwanao😀 its Football Wanangu mchezo wa wazi sana, timu nyingi duniani zinapambana kupata Makipa ambao ni Sweepers, watu wanataka Wachezaji 11 na sio 10 wa ndani tena. 


VISIT MOROGORO🇹🇿

Post a Comment

0 Comments