Kama timu bado ni wageni kwenye mashindano ya Afrika, kwao huu ni mchakato wa kujifunza na kuona mambo yanaendaje, nini wanapaswa kufanya na kipi hawatakiwi kufanya. Bado wapo kwenye hatua za ukuaji.
Ndio kwanza wamecheza mechi tatu tu za mashindano ya Afrika tangu kuanzishwa kwao na leo watacheza mechi yao ya nne wakiwa ugenini kwenye taifa kubwa kwenye maendeleo ya soka lakini pia dhidi ya mpinzani mgumu, tuwaache Singida waendelee kujitafuta.
Kwa hiyo kwa Singida Fountain Gate FC kundi kubwa la watu ni wageni kwenye mashindano kuanzia wachezaji, benchi la ufundi hadi viongozi wao! Tuwaache wapate shule, kama watashiriki mashindano haya mara kwa mara badae tutaanza kuwadai.
Ikitokea wamefuzu hatua ya makundi ni jambo zuri na jema kwao na kwa soka la Tanzania [bonus], ikitokea hawajafanikiwa ni tusiwanyooshee vidole vya lawama utadhani ni timu ambayo imeshawahi kufika hatua za juu lakini leo imeshindwa kufuzu makundi.
Wanachotakiwa kufanya Singida Fountain Gate ni kuwa na ‘consistence’ ya ushiriki wa mashindano ya CAF kwa maana ya kumaliza nafasi za juu kwenye Ligi yetu ili kupata nafasi za ushiriki wa mara kwa mara ambao sasa utawapa uzoefu kwenye mashindano hayo.
Kila la heri walima alizeti🌻 kila la heri Tanzania 🇹🇿
0 Comments