Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SINGIDA IMEPOTEZA ILA KWA MECHI HII HAKUNA WA KUMLAUMU

 


.

✍🏻Singida FC bora hata hii mechi isingeoneshwa tungesema mmeonewa lakini tumeona vizuri tu , kiukweli level ya kiufundi ya mchezaji mmoja mmoja 

1: Jinsi ya kupokea mali 
2: Jinsi ya kulinda mali 
3. jinsi ya kupiga pasi sahihi katika sehemu sahihi
4: Movements 

Tuseme tusemavyo makosa ya Singida FG lakini hayo makosa yalihitaji kuadhibiwa ndio yaonekane . 

✍🏻Muda ambao Singinda FG walicheza vizuri ni ule muda ambao walikuwa nyuma 1-0 

1: Fullbacks wote walikuwa wanasogea juu kuwapa fursa wingers wao kushambulia ndani 

2: Viungo wawili wote wali push juu karibu na mstari wao wa washambuliaji 

3: Ndio maana iliwasaidia kutengeneza presha na mashambulizi mazuri . 

✍🏻Sasa basi baada ya kadi nyekundu ya Future FC , aisee Singinda FG walipigiwa boli bhana utasema Future FC wapo wengi dimbani . Walifanya kila kitu kwa usahihi 

1: Defending ✅
2: Third man runs ✅
3: Tanua uwanja licha ya kuwa pungufu ✅
4: Vuta subira ✅
5: Tumia mpira vizuri , usipoteze mali kirahisi✅
6: Toa adhabu kwa kila kosa linalofanyika ✅

NOTE 

Hii note ni kwa ajili ya mchezaji mmoja tu AHMED ATEF ... ni nani alisema kucheza kama mshambuliaji mmoja mbele lazima uwe mrefu na mwili nyumba ? 

Huyu mwamba :- 

1: Fundi mguuni 
2: Anajua kulinda boli 
3: Kasi yake kama haendi vile ( deceptive quick)
4: Ana jicho la pasi 
5: Uwezo wa kucheza goli la timu pinzani kulipa mgongo 
6: Mzuri hewani licha ya kimo cha kawaida 

Amewavuruga sana Carmo na Hamad .! 

FT : Future FC 4-1 Singida FG ( Agg: 4-2 ) 


Post a Comment

0 Comments