✍️ Kuna kitu nimekiona ndani ya timu hii ya Simba SC ambacho pengine sikukiona kwenye msimu uliopita. Kitu hicho ni ile hali ya kuyataka matokeo chanya katika nyakati ngumu.
Mechi kama ya leo pengine ingeisha kwa sare msimu uliopita.
✍️ Simba ilikuwa ikipata taabu sana kwenye mechi ambazo pressure yake kutoka kwa wapinzani ni kubwa kwenye msimu uliopita lakini kwa msimu huu hali ya kulazimisha matokeo imeongezeka na hapa mwalimu tumpe maua yake.
✍️ Simba wamefurahia sana goli la pili kwasababu mbili kubwa. Moja, ni goli la ushindi hivyo lina utamu wake, lakini pili, limefungwa na nyota kipenzi chao MOSES PHIRI. Huyu anapendwa sana na Wanasimba. Bila shaka goli kama hili linazidi kumrudishia hali yake na ule ubora wake taratibu.
✍️ Simba SC wanakusanya alama tatu taratibu halafu wanakwambiaje "TUKUTANE MWISHO WA MSIMU".
We cheza vizuri tu ila tukutane kwenye msimamo😅
SIMBA HAOOOOOOO🔥🔥
0 Comments