"Viingilio tumepanga kwa kuangalia hali za watu wetu.
Platinum - Tsh. 200,000
VIP B- Tsh. 40,000
VIP C - Tsh. 30,000
Machungwa - Tsh. 10,000
Mzunguko - Tsh. 7,000.
Hatutakuwa na VIP A sababu jukwaa limechukuliwa na FIFA na CAF."
"Tiketi tayari zimeanza kuuzwa vituoni."
"Tutazunguka Dar nzima kufanya hamasa. Tarehe 14 ndio tutazindua wiki ya Kispika (Wiki ya Hamasa), tutazindulia Coco Beach. Kutakuwa na matukio mbalimbali kama mechi za mashabiki na pia kutakuwa na watu wa kuuza tiketi, watu wa NMB na CRDB kwa ajili ya watu kupata namba za mashabiki lakini pia jezi zitauzwa pale."
"Hii ni wiki yetu, kama kuna mtu kinamkera aende hata Tanga. Hiyo tarehe 14 tutaanzia maandamano kutokea makao makuu ya klabu kwenda Coco Beach. Tunatarajia kufika Coco majira ya saa 4 asubuhi."
"Jumapili itakuwa mapumziko kidogo. Jumatatu tutakuwa na Paint the City, hiyo siku ni kubandika vipeperushi kila sehemu. Kwenye mstimu, kwenye geti, kwenye magari. Hakuna mtu ambaye hatajua kama Simba inacheza tarehe 20."- Ahmed Ally. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja
0 Comments