"Ni tukio jipya duniani, Afrika na hata Tanzania. Ni tukio pekee lenye thamani zaidi ndani ya wiki hizi mbili barani Afrika. Hii ndio michuano mikubwa zaidi barani Afrika na inashirikisha watu bora pekee na watu bora Tanzania ni Simba SC."
"Halijaja kwa bahati mbaya, ni kwa juhudi ambayo Simba imeifanya. Wakati wanapanga timu za kushiriki waliangalia timu zenye thamani na ubora. Kwanini Simba Sports Club ni sababu ya ubora wetu. Kila Mtanzania aseme asanteni na hongera Simba SC."
"Hili sio jambo la kawaida na sio tu mchezo lakini ni ufunguzi wa michuano hii. Hili ni jambo kubwa zaidi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu Tanzania."
"Hii ni African Football League ya kwanza duniani, mwakani na miaka ijayo timu zitaongezeka zaidi ya nane hivyo thamani yake haitakuwa sawa na sasa. Ni aibu siku hiyo uwanja ukiwa haujaa. Sio siku ya mtu kukosa."- Ahmed Ally. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja
0 Comments