Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MFAHAMU HERON RICARDO FERREIRA...KOCHA MPYA SINGIDA FOUNTAIN GATE


Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate imemtangaza RICARDO FERREIRA almaarufu kama HERON kama kocha wao mkuu mpya. 

Kocha Heron sasa ndiye atakayekuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu hiyo akichukua kiti cha mtangulizi wake ERNST MIDDENDORP.


Ni nani huyu HERON RICARDO FERREIRA??

Huyu ni Mbrazil mwenye umri wa miaka 65 na mzaliwa wa Rio de Janeiro.


Katika kazi yake kama kocha wa mpira amefanikiwa kupita katika vilabu kadhaa barani Afrika na kuacha legacy ya kueleweka

Amepita pale Ismaily ya Misri na kuwa mshindi wa pili kwenye ligi kuu ya Misri.

Akapita Al Hilal ya Sudan na kuchukua ubingwa wa ligi mara tatu pamoja na kuifikisha klabu hiyo nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika.


Siyo hivyo tu kwani kocha huyu alikuwepo pia pale Al Mereikh ya Sudan pia na kuwapa ubingwa wa ligi, kuwafikisha nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na makundi ya klabu bingwa kwenye msimu wa 2022/23.


Wasifu wake kwa vilabu vya ndani ya Afrika ni mkubwa hivyo ni kocha mkubwa... 


Na akawe na wakati bora ndani ya Singida Fountain Gate




 

Post a Comment

0 Comments