Kuna historia nyingine ni ngumu sana kuzivunja. Ni kama hii historia ya Simba na mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Ni historia ya kuvutia sana. Nimeona kelele nyingi sana huko mitaani kwa baadhi ya watu wakijinasibu kuwa, wao ndio wababe kwenye mashindano hayo. Inashangaza sana. Ukweli upo wazi.Simba ndio timu ya kwanza nchini kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya CAF. Ilianza 1974 na inafanya vizuri hadi leo.
.
Mwaka 1974 ilifika nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa). Ndio rekodi ya kwanza kubwa kwenye mashindano ya Afrika kuwekwa na timu ya Tanzania. Ilikuwa ni kama nyota inayoanza kuangaza kwa Simba. Miaka 19 baadaye ikafika fainali ya Kombe la CAF (michuano iliyoungwanishwa na Kombe la Washindi na kuwa Kombe la Shirikisho Afrika la sasa). Ikawa timu ya kwanza kwa Tanzania kufika fainali ya mashindano hayo.
.
Baada ya Simba kufika fainali mwaka 1993, imechukua miaka 30 kwa timu nyingine ya Tanzania kufika katika hatua hiyo. Ni Yanga ambayo imefika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kukosa kiduchu kubeba taji kwa kanuni ya bao la ugenini licha ya matokeo yote kuwa sare ya 2-2.
.
Yaani wakati Simba inacheza fainali ya CAF mwaka huo, hawa vijana wadogo wanaopiga kelele mitandaoni walikuwa hata hawajazaliwa. Sio kuzaliwa tu wala ilikuwa haijulikani kama watazaliwa la ajabu ni kwamba leo wanakuwa wa kwanza kukashfu fainali ya Simba
Inaendelea….
0 Comments