SIMU YA PROFESA KUHUSU SIMBA SPORTS CLUB.
Profesa kanipigia simu tumezungumza mambo kadhaa kuhusu SIMBA baada ya mchezo wa leo, naye alikuwa na maoni yake ambayo anaamini yapo sahihi.
MEDIA, Katika kitu ambacho Kijana wangu mtakubali ama mtakataa ila Waandishi mnachangia pakubwa sana kuifikisha Simba ilipo leo hii, hamkosoi inapostahili mtasaka maneno laini kuuficha ukweli, matokeo yake Viongozi wanatembelea kivuli hicho ila ni ukweli kuwa Simba haijapiga hatua, inatembelea project ya miaka minne nyuma ambayo ipo mwishoni.
Mmekuwa wepesi kutafuta majibu rahisi hata katika hoja nzito, wamefeli kwenye sajili kadhaa ila Media mnapaka rangi upepo, wamefeli kuunda project mpya ila mnapaka rangi upepo, semeni ukweli na ninyi ndio msaada kwa hii timu, Mashabiki wanafahamu ukweli ndio maana wenyewe wameamua kuipigania timu yao, Media mmechangia sana.
UTAMADUNI, Farhan niliona clip yako ukitoa takwimu za pass mara mpira umebadilika zama hizi! Nikuulize swali ni zama hizi kuna timu zilikuwa zinacheza direct football ila sasa wanacheza mpira mzuri, kwanini Simba ahame kwake na kwenda ambapo sio kwake?
Mashabiki wanalilia identity yao! Mwingine aliipenda Simba kwasababu ya mpira mzuri, nikukumbushe SIMBA enzi za UKAWA? Timu ilikuwa haishindi ila mpira unapigwa sana, maswali yanakuwa magumu timu imewekeza lakini ipo down! Hata mfumo mpya waliohamia bado hauridhishi, kwanini wasiumie Mashabiki!?
MASLAHI, hii Simba ina shida kuna baadhi ya Mashabiki wanajipa mwamvuli wa Uhafidhina wao hakuna baya la Viongozi, Mashabiki wanaokosoa wanapewa majina mabaya, hawataki mawazo kinzani ambayo ndio msingi wa taasisi imara, niliwahi kuwafundisha Chuoni kwenye EDUCATION MANAGEMENT (EA 200) niliwaambia ustawi wa taasisi yoyote ni lazima MIGOGORO iwepo, shida ya Simba hiki kitu Wahafidhina hawataki.
Mfano lile goli ni uzembe wa Wachezaji, akitokea Shabiki akiwaita Wazembe linakuwa kosa? Mfano suala la Kipa, Beno anamalizaje mkataba quality yake na huumpi mkataba unaenda kubet langoni? Lini mtasema kuhusu hii blunder ya Viongozi ambayo inaitesa timu? Mnafahamu kuwa dirisha la usajili mkaenda kujaza wachezaji wengi waliofanana? Ilikuwa ina maana gani?
PROFESA.
0 Comments