.
✍🏻Ndio uwanja nyasi za kijani lakini hali yake hairuhusu sana kucheza pasi za chini ( kuweka mali chini ) lakini Simba SC bado walitafuta namna ya kuwa bora uwanjani zaidi ya TZ Prisons
✍🏻Baada ya Simba SC kufungwa goli , jinsi walivyo react ndio kocha yoyote anavyotaka
1: Hakuna kushusha mabega chini na kujionea huruma
2: Hakuna haja ya kupaniki
3: Tuongeze idadi ya wachezaji wa kushambulia
4: Tusiwape Prisons wanachokitaka ( ambacho kucheza mipira ya juu mingi )
5: Muundo wao wa ulinzi pale ambapo wana mpira ili kukabiliana na counter attacks ulikuwa mzuri
6: Hakikisha unajizuia kufanya faulo zisizo za lazima kuwapa Prisons silaha wanayoipenda
✍🏻Baada ya hapo , Prisons wakaanza kuwa watumwa , sasa ilikuwa zamu yao kuonesha wanarudi vipi mchezoni lakini kwao ilionekana plan yao ni moja tu ... weka mali ya juu kwa akina Mbangula , shinda mpira wa kwanza na ikiwezekana wa pili lakini , uzuri kwa Simba hata kama mpira wa kwanza waliukosa basi walihakikisha ule wa pili ulikuwa wao .
✍🏻Dakika kama 20 za mwisho , Simba SC waliwapa Prisons ladha ya dawa yao , kaa nyuma na cheza kwenye counter attacks wakiamini wanao wachezaji wenye madhara ( Bocco , Chama , Saido na Kibu ) na ndio maana walikuwa wakifanya hivyo wanaonekana hatari kwa Prisons . ( Game Management ✅)
NOTE
1: Ile presha ya Simba SC baada ya kufungwa goli , nafikiri iliwazidi maarifa Prisons
2: Freekick Balua Jr 🔥 hakuna namna Salim anaokoa
3: Kennedy bhana kama vile nyota yake haing'ai lakini kila akipata nafasi ya kucheza huwa anakupa performance nzuri tu .
4: Prisons wapo walipo kwa sasa kwenye msimamo kwasababu wanashindwa kufunga duka vizuri , makosa mengi sana na adhabu lazima ipatikane
5: BADO HAWAJASEMA ???
FT: TZ Prisons 1-3 Simba SC
0 Comments