Mmenionea wazi wazi tena Mchana kweupe, Mkanidhulumu kwa kunipa adhabu kubwa ya kikatili na sasa mna kampeni ya kufuta jina na Legacy yangu.
Hata yale mema niliyoyafanya ktk hamasa ya Soka la Tanzania mnataka kuyafuta!!
Mnataka hadi kuhalalisha hii dhulma kwa kudai eti mimi nilikuwa Rafiki yenu, toka lini tushawahi kuwa Marafiki kwa namna yoyote ile, yaani kuhalalisha hiii dhulma iwe hadi kunisingizia urafiki? Too Much wakubwa.
Mmeshaamua kunionea Basi niachieni maisha yangu lakini sio kuendelea kuchafua taswira yangu daily, mnanifanyia hivi utadhani nimeua au kweli nimemtusi mtu? Au mimi Sio Mtanzania labda, Yaani naonewa ndani ya Nchi yangu na muoneaji anatoka public kuhalalisha dhulma?
Soon ntakuja hadharani kutangaza kuachana na kila kitu kuhusu Football isije kutolewa uhai wangu nikaacha familia yangu bila sababu, najua hapo mtafurahi na mtaniachia maisha yangu yawe salama.
Serious Kiongozi mkubwa kama huyu anatoka hadharani kusema nimeikosea Taasisi, ilhali jambo hili limetokea mbele ya Umma na Viongozi wakubwa tu wakiwepo?
Tanzania tumefika huku? Ndio hivi vyeo vinatupa nguvu hiyo ya kudhalilisha wenzenu ili tu mpate utukufu?
Ok ;; Tumuachie Muumba Mbingu na Ardhi ipo siku atatenda lililo sahihi Insha'Allah 🙏🏻🙏🏻
0 Comments