Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HAJI MANARA AANDIKA MAZITO KWA MASHABIKI WA YANGA NA BEKI WAO MWANYETO, JOB NA BACCA ANAGALIA


Kwa Wanayanga Wenzangu 


Kuna kitu tunapaswa kukiseme kwa ukubwa wake na tunatakiwa kutoa heshma inayostahili kwa Viumbe hawa Watatu!!


Hivi huwa tunaangalia vizuri performance ya Utatu huu wakicheza pamoja wote au wawili miongoni mwao? Mnajua hawa Wanaume ndio kila kitu pale nyuma na ndio wanaotufanya tutembee vifua mbele mtaani? 


Wanaishep team yetu na kuwafanya Viungo na Washambuliaji wetu wawe bora kila siku, Wanatengeneza Chuma kisicho na kutu ndani ya team hususan kwenye Backline yetu.


Ulinzi wao kwa Kipa la Afrika na wenzie ni wa kiwango adhimu mno kiasi cha kwamba Makipa wetu wanaendelea kushine everyday!!


Tuwaimbe na Tuwataje kwa nguvu ile ile tunaowataja na wengine, Achana na Utanzania wao lakini kwa wanachotupa tunastahili kujivunia sana na wao, itawaongezea morali zaidi na itawafanya thamani yao izidi kukua!!


Ni mbinu bora ya kuwafanya waongeze mapenzi yao kwa team, kuwaimba na kuwataja taja positive mara kwa mara, kuwaambia kuhusu ubora wao, kuwaonyesha kuwa wao ni much better kuliko kina Maguire au kina Puyol !!


Sikumbuki kama Nchi tushawahi kwa wakati mmoja kuwa na Top Central Defenders Watatu wenye ubora huu na wanaocheza team moja, imbeni kuhusu wao, semeni kuhusu wao,wapeni sifa zao na jivunieni sana wao.


Itawajenga zaidi katika kujiamini na Always Confidence ndio hujenga zaidi Quality ya Mchezaji.


By the way, hawa ndio tegemeo letu kule Afcon mwakani, tujivunie sana wao na tusione haya kusema kuhusu ubora wao.


Kama hujanielewa leo, one day utanielewa kuhusu mbinu hii ya motivation kwa Wachezaji wetu, always hulipa.


@mwamnyeto03 @jobdick05 @ibrahim_bacca
 

Post a Comment

0 Comments