Jana nilikuwa miongoni mwa watanzania niliyeshuhudia Taifa Stars ikifuzu michuano ya AFCON mwakani 2024 katika ardhi ya ALGERIA mbele ya nyota wao wakubwa wanaosakata kabumbu Ulaya
Jasho na damu lilikuwa kwa kila mchezaji wa Stars aliyevaa jezi ile huku akijitoa kwa asilimia zote ndani ya dakika 90 za mchezo, sikuona mchezaji akizubaa pindi walipopoteza mpira na kukaa katika maeneo sahihii
Nitapongeza benchi la ufundi la Stars kwani alionyesha kushirikiana kwa kuhimizana wao kwa wao muda wote na ilifika wakati walidiriki hata kuwapa presha waamuzi wa mchezo ule kuwakumbusha dakika zimekwisha wamalize mchezo
Hii ni Stars yetu isitokee zikaanza Stori nani kafanya zaidi ya mwingine kwasababu tu timu imesonga mbele, huu ni muda sasa kama Taifa kujipanga kuona tunakwenda vipi kuyaanza hayo mashindano ya AFCON
Asante Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu kwani umekuwa chachu muda wote na umejitoa kweli kweli kweli huu upande wa michezo na imeonekana wazi hapo kwa kutimiza ile ahadi yako ya Shilingi Milioni 500 pindi tu timu itafuzu na WIZARA ya michezo imelithibitisha hilo kuwa wameshazipokea pesa hizo
Kama Watanzania tujiandae kwenda airport kuipokea timu tukajazane tukaimbe kwaajili ya jambo hili KUBWA nchini
0 Comments