Vitu ambavyo nimeona leo hasa kimbinu
✍🏻Atletico walikuwa wanatumia sana " A third man runs " na iliwapa tabu sana Real Madrid
1: Wingbacks wao ( Molina na Lino ) pembeni ya uwanja na kunyakati walikuwa wanafanya movements nzuri sana za kuwa third man runners na mara nyingine kuwa wingers
2: Viungo wao wa kati kulia na kushoto ( LCM + RCM ) Saul na Llorente energy yao ya kushambulia space baina ya mabeki wa kati wa Real na fullbacks wao
✍🏻Kuna nyakati kwenye build up ya Atletico nilivutiwa na majukumu ya Hermoso ambaye yupo kati ya mabeki watatu wa nyuma wa Real , alikuwa anasogea juu kwenye kiungo kuungana na Koke kuwa namba 6 wawili . Maana yake ?
1: Kuwazidi idadi ya viungo Real ambao walikuwa na viungo wanne ( Kroos Fede Modric na Camavinga ) wao walikuwa watano kwasababu Griezman alikuwa anashuka chini ( Griezman Saul Llorente Koke na Hermoso )
✍🏻Dakika 15-20 za mwisho katika kipindi cha kwanza Real Madrid walionekana kupata tiba nzuri dhidi ya 5-4-1 ya Atletico kwenye kuzuia
1: Kutengeneza combinations pembeni ya uwanja ( Fran Garcia + Bellingham & Fede + Lucas )
2: Camavinga na Modric walikuwa wanashambulia space baina ya Outside CBs wa Atletico ( Savic na Hermoso ) na wingbacks wao ( Lino na Molina )
3. kroos kazi yake ilikuwa kudumisha umiliki wa mpira kwa Real Madrid maana yake Atletico walikuwa wanapata tabu kutoka nyuma .
NOTE
1: Siku zote ukiruhusu mshambuliaji kusoma namba yako ya jezi upo matatizoni ( magoli yote matatu ya Atletico yamekuwa hivyo )
2: Ule mkwaju wa Toni Kroos 🔥
3: Lino kila akiwa na mali , Lucas Vazquez/ Nacho wanajua shida inakuja 🔥
4: Morata hewani 🔥
5: Rodryigo alijitahidi sana kuwa busy msumbufu 🔥
FT: Atletico 3-1 Real Madrid
0 Comments