Hot Posts

6/recent/ticker-posts

UMRI WA MZIZE MIAKA 19 ILA AKILI KUBWA KWENYE MECHI KUBWA


🗣️ Clement Mzize kwa sasa ameonyesha kwamba anahitaji kuaminika na kupewa nafasi zaidi kuanzia kwenye klabu yake na timu ya Taifa ya Tanzania 🇹🇿 

🗣️Kumekuwa na kasumba klabu sana kwa wachezaji vijana ambao wamepanda kutoka katika klabu zetu kongwe za Simba na Yanga kwenye kuonyesha ubora walikuwa wanaonyeaha katika timu za vijana endapo watapanda timu kubwa, Lakini kwa Mzize amepambana kwa nafasi kubwa kuakikisha anaoyesha uwezo katika timu kubwa na kupewa nafasi ya kudumu katika kikosi

🗣️Leo klabu ya Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi katika kombe la klabu bingwa barani Africa baada ya kupita miaka 25, Hii inamaana kubwa katika soka la Tanzania na klabu ya Yanga kwakua bao la ushindi limefungwa na Mchezaji aliyekuzwa na kulelewa na klabu ya Yanga, Hivyo ni nafasi kwa klabu zetu kuhakikisha wanawekeza sana katika soka la vijana na kutengeneza mipango ya maana kwa manufaa ya klabu na soka la Tanzania kwa ujumla



 

Post a Comment

0 Comments