UMEBURUDIKA ?
✍🏻Hii mechi kwa Coastal Union iliisha kabla ya kuchanganya vizuri , hata bila kadi nyekundu bado Simba SC walionekana imara zaidi ya Coastal katika kila kitu na kila eneo . Wamefungwa magoli matatu yenye sifa mbili tofauti
1: Turn Over
2: Rotations
✍🏻Goli la kwanza Simba lilitokana na " Forced Turnover " yani kwamba Simba walilazimisha kurejesha mpira kwenye himaya yao kutoka kwa Coastal ( Lawi kufanyiwa pressing na kupoteza mali )
✍🏻Magoli mawili mengine ni yanahusu Rotations ya wachezaji uwanjani hasa hawa watatu ( Chama , Saido na Miquissone ) jinsi walivyokuwa wanabadilishana nafasi uwanjani ilikuwa ngumu kwa Coastal kukabaliana nao maana hawakujua nani kutoka kwao anatakiwa kukabiliana na nani kati ya hao watatu mpaka Simba kuwafungua ( Penati na win rebound Zimbwe Jr )
✍🏻Nafikiri baada ya kadi nyekundu , kwa Coastal ilikuwa kupunguza idadi kubwa ya magoli ya kufungwa kwa kufanya hivi vitu viwili vya msingi sana ukiwa pungufu
1: Zuia kwa idadi kubwa ya wachezaji hasa ndani , kubali kuruhusu krosi
2: Kaa na mpira pindi unapoupata kwa muda mrefu iwezekanavyo na kama kuupoteza basi upotezee kwenye zone ya mpinzani wako sio kwako
✍🏻Kwa Simba SC kwao waliona ni kutunza energy yao , upo mbele magoli matatu , dhidi ya timu ambayo ipo pungufu uwanjani haina haja tena ya kukimbizana nao ili kuepusha majeraha au kutumia energy zaidi wakati kuna ratiba zingine zinakuja ( Game management ) vuta subira , pasiana sana , ikitokea nafasi ya kufunga fanya hivyo .
NOTE
1: Hat Trick ya Jean Baleke , hakuna raha kama ukiwa kwenye presha ya baadhi ya mashabiki halafu unakuja kupiga hat trick 🔥
2: Ajib huwa inaonekana ana enjoy sana kucheza chini ya Mwinyi Zahera
3: Pasi za Fabrice Ngoma ni elekezi , zinamuambia mpokeaji anatakiwa kufanya nini baadae
4: Yes , tunapenda sana kucheza kuanzia nyuma lakini muda mwingine fanya vitu rahisi ( Lameck Lawi ) alizidisha sana na credit kwa Simba kumpora mpira
5: Get well soon Inonga 🙏🏻
FT : Simba SC 3-0 Coastal Union
0 Comments