Ni rasmi sasa tutashuhudia michuano mikubwa zaidi kwa ngazi ya timu za taifa barani Afrika ikichezwa kwenye ardhi yetu ya Tanzania na kwa majirani zetu Kenya na Uganda. Ni michuano ya mataifa bingwa Afrika (AFCON2027). Hii ni ya kwetu Afrika Mashariki.
Kwanini tuna deni??... Deni linatoka wapi???
Hili ni deni la miundombinu kwenye nyanja zote lakini kubwa zaidi ikiwa ni kwenye eneo la viwanja vya kufanyikia michezo yenyewe ya hadhi ya AFCON.
Sijui kwa majirani zetu Kenya na Uganda lakini kwetu bado tuna shida kwenye eneo hilo ingawa jitihada kubwa zinafanyika.
Tunatakiwa kufanya kazi kweli ili michuano ikifanyika iwe rahisi kwa wakati mwingine kuomba nafasi hiyo na tukapewa. Tusifanye watu wakajuta kutupa hiyo nafasi kitu ambacho kitafunga milango ya kupata nafasi kama hiyo kwa miaka ya mbele zaidi.
Jitihada kubwa sana zimefanyika na taasisi husika mpaka tumepata nafasi hii na sasa ni nafasi ya mamlaka husika chini ya serikali kuzipa sapoti mamlaka za soka husika kufanikisha hili.
AFCON 2027 ni ya kwetu✊
0 Comments