Hot Posts

6/recent/ticker-posts

PAMBANO LA HAASAN MWAKINYO KESHO BADO MASEKE


CHAMPEZ MWAKINYO anapambania standard kwenye game ya boxing kwa mujibu wa chanzo ni kuwa Promoter wa hii fight kuna vitu havipo sawa kwa mujibu wa makubaliano yao. 


- Kubadilishiwa Bondia, yes alipaswa kupigana na Okwiri, Hassan akatrain vyema lakini wiki moja kabla akaambiwa kuwa Bondia huyo ameumia kwahiyo atabadilishiwa Bondia, Hassan alikubaliana na hilo na akaanza kutrain kwa Bondia mpya waliyompangia, shida sio Bondia kubadilishwa. 


- Promoter kuvunja makubaliano, Kuna taarifa kuwa Promoter wa hii fight alipungukiwa pesa hivyo akashirikiana na Promoter mwingine ili pambano lipigwe, Hassan baada ya kusikia hivyo aliwasiliana na Promoter na kumwambia kama changamoto ni pesa basi yeye atatoa zake kuongezea ili pambano lipigwe pasi na kulihamishia kwa mwingine, inasemekana alipokea mzigo huo Promota. 


Nikajaribu kufuatilia kwanini Hassan alikataa Promota asimpe Promota mwingine? Ni kuwa Hassan alishawahi kupishana kibiashara na huyo Mtu hivyo kiamani hakutaka ahusike kwenye biashara yake, hakutaka hata Mabondia wake waje kwenye pambano lake. 


Kwakuwa Hassan alishatoa mzigo kwa Promota ili pambano lipigwe bila kutafuta mwingine wa kumsaidia, leo hii anashangaa kwenye kupima uzito anakutana na sura ambazo alizikataa ikizingatia kuwa alishatoa hela zake kuongezea, ndipo hapo shida ilipoanzia. 


Yaani Promota alipungukiwa pesa akataka kuuza Pambano kwa mwenzake ambaye hawaivi na Hassan, Champez akagoma akaongezea hela yake halafu ghafla anakutana na sura alizozikataa leo kwenye kupima uzito. 


Kwa mujibu wa chanzo changu, Hassan amekutana na Azam Media usiku huu maeneo ya Don Bosco ambao wao ndio Broadcasters, wanataka kuliweka sawa kati ya Hassan na Promoter, kama vitu vitaenda sawa basi fight kesho itakuwepo kwa mujibu wa chanzo changu. 


Hassan hana shida na Bondia kubadilishwa bali masuala ya kibiashara. 


VISIT MOROGORO🇹🇿
 

Post a Comment

0 Comments