Hot Posts

6/recent/ticker-posts

"Mjadala wa Shomari Kapombe na Mohamed Hussein: Mtazamo wa Kwa Kina Kuhusu Vipaji vya Ulinzi vya Simba na Mkakati wa Kocha"


Naomba nizungumze kama Shabiki lakini pia kama Mwandishi wa Habari, nimeona mjadala kuhusu Shomari Kapombe na Mohamed Hussein, naona baadhi wanataka wapumzishwe kwamba wamechoka sana, nimeona baadhi wanasema wanafanya sana makosa na wengine wanasema Vijana ni wakati wao wa kupewa nafasi.

Maoni ya kila Mtu lazima yaheshimiwe lakini tujihoji kwanini Mwalimu amechagua kuwatumia zaidi? By default hizi ndio mbavu bora zaidi nchini kwa Wazawa tena kwa kilometa nyingi sana, huwezi kureplace talents kama hizi kama kubadili boxer, huwezi kubadili nafasi zao ghafla.

Em nitajieni mechi ngapi wameharibu? Ni ghafla sana mjadala umeanza.

Itazame kwanza ratiba ya Simba! Mechi mbili ngumu za Ngao, dhidi ya Yanga na Singida pale Tanga! Ukuta huu haukuruhusu bao lolote, ni ngumu kurotate talents kama hizi! Wakaja mechi mbili ngumu za Ligi Kuu kisha mechi ngumu ya Champions League, nani anataka Mwalimu acheze kamari kwa nyakati ngumu kama hizi?

Kuhusu Vijana kucheza kifupi watacheza tu sana! Simba tuna CAF SUPERLEAGUE, Champions League, Ligi Kuu, FA Cup na Mapinduzi yote haya wachezaji watapewa nafasi na watacheza! Hakuna haraka hiyo! Hawajaletwa Simba kuja kuwatoa Kapombe ama Zimbwe bali kucheza mpira na muda ukifika watacheza, ukweli ni kuwa wanaoanza wanawazaidi parefu, wao wanachipukia waendelee kujifunza.

Mwingine anasema hawa wamecheza sana! Sasa kazi ya Mchezaji ni nini? Sio kila eneo utabadili tu, Marcelo kazima sana Real, Dani Alves kazima sana Barca sio kwamba wengine hawapo ama Messi na Ronaldo, Mwalimu anatazama unachofanya mazoezini na sio hoja ya kutumika sana, hoja ni product yako.

Mind you! Mnawaandalia presha bure Vijana! Mnawapa mlima mzito siku wakipata nafasi na kinachowaumiza mara zote ni watu sasa kutaka kuwafananisha! Mwacheni Kocha afanye anachoona ni sahihi na atawapa namba wakati sahihi, waendelee kujifunza na nafasi ipo kwakuwa kuna majeraha, kuna rotation na michuano ipo mingi.

Khalid Aucho hukuona anafanyiwa rotation kila mara, Fiston Mayele hukuona anakosekana kila mara, mechi nzito Diarra atakaa langoni, Stephen Aziz Ki atakaa nje mechi ngumu? Come on Guys its football!


Post a Comment

0 Comments