✍🏻Mtu akiona matokeo anaweza kuhisi mechi ilikuwa tight sana lakini ni Bayern ambao wakiamua kufunga basi unaona goli lileeee linakuja . United wakifunga basi Bayern kama vile wanasema " tunakuja kufunga goli letu tena " BANG .!
✍🏻United walianza mchezo vizuri jinsi walivyokuwa wana press na kuwalazimisha Bayern kupoteza mipira hasa pale walipokuwa wanataka kutoka nyuma
1: Bayern walikuwa wanafanya build up na 2-3 ( Upamecano na Kim ) nyuma na mstari wa Laimer Kimmich na Davies
2: Lakini United walikuwa wanafanya pressing kwa 4-1-4-1 Hojlund anafunga njia ya pasi kwa Kimmich huku Rashy na Pellistri kwa Fullbacks wote wa Bayern : Bruno na Eriksen wanafunga njia za pasi zinazopita kwenye halfspaces zote mbili kwasababu ya Musiala na Goretzka .
✍🏻Bayern baada ya kutulia na kuanza kupasia mpira vizuri , ndio shida ilipoanza kwa United
1: Musiala anakuwa maeneo ambayo anajua Casemiro na Eriksen hawawezi kufika na anajua akishapata mpira ni rahisi kupita katikati yao
2: Kane anashuka chini kidogo ili kufanya kazi ya Lisandro na Lindelof kuwa ngumu , kwasababu wakimfuata wanaacha space nyuma yao kwa Sane na Gnabry kuishambulia , wasipomfuata anapokea mpira na kupiga pasi kwa wingers wake
✍🏻Aina ya magoli ambayo United wanaruhusu yanafanana sana msimu huu
1: Goli la pili dhidi ya Spurs
2: Goli la Martin Odegaard
3: Magoli yote ya Brighton
4: Goli la Gnabry
Yanafanana nini ? United wanashida sana ya kukimbia na runners wa timu pinzani ( tracking runners ) , cutbacks zinawafunga sana United msimu huu na timu zinajua hilo . Casemiro na Eriksen pamoja kwenye kiungo bila mpira ? 🤔🤔
NOTE
1: Jamal Musiala kawapika sana viungo wa United
2: Kimmich muda wote anapicha kichwani kwake nini kinaendelea na nini afanye
3: Bayern bila mpira wanaacha space nyingi sana ni wewe tu kuwapa adhabu kama unataka
4: Goli la nne la Bayern , pasi , movement na finishing 🔥
5: Andre Onana wakati anaopitia sasa hivi 🤔
6: Man United katika mechi 5 zilizopita wameruhusu magoli 14 🤔
7: Kufunga magoli 3 ugenini na bado hujashinda mechi 😭
FT: Bayern 4-3 Man United
0 Comments