Kocha wa timu ya Taifa ya Uganda Milutin Sredojevic Micho, naweza kusema ni kama hajatenda haki kwa beki kisiki wa Yanga SC, Gift Fred
Kwanza ameivunjia heshima klabu kubwa hapa nchini YANGA SC kwani imeleta taharuki wengine wakiamini klabu hiyo ilitoa taarifa ya uongo kuitwa kwa mchezaji wao kwenye kikosi cha Taifa ya Uganda
Micho sijui alikuwa ana maana gani kumuita mchezaji na baadae kumtema kwa kigezo cha eti hakuwa fiti.... nafikiri haikutumika busara kwenye hilo
Gift Fred ni mchezaji mzuri japokuwa kwenye kikosi cha Yanga anaanzia benchi na hilo linaeleweka kwani aliowakuta wapo kwenye fomu kwaiyo inakuwa ngumu ya yeye kuanza moja kwa moja
Na hii inaenda kumvuruga hata mchezaji mwenyewe kwani wote tunafahamu ukiahidiwa jambo halafu likakatishwa namna unavyojisikia
Pole kwake Gift Fred, pole pia kwa uongozi wote wa Yanga SC kwa kuchafuliwa kwa njia hiyo imani yangu mambo yatakaa sawa
0 Comments