✍🏻Liverpool leo wamefanya kila kitu cha msingi kwa usahihi sana dhidi ya Aston Villa
1: Pasia mpira vizuri
2: Rudi kuzuia haraka ( recovery runs )
3: Weka presha kwenye mpira
4: Fanya runs nzuri katika wakati sahihi
5: Malizia nafasi zako ulizotengeneza
✍🏻Jurgen Klopp leo alibadilisha kidogo kuhusu TAA Liverpool wakiwa na mpira katika phase mbili za mwanzo
1: Phase ya kwanza wanakuwa 4-2 ( TAA Matip Gomez na Robbo mbele yao Mac Allister na Szobo )
2: Phase ya pili wanakuwa 3-2 ( Matip Gomez na Robbo na mbele ya Mac Allister na TAA )
Kwanini hivi ??? Kwasababu Klopp atakuwa alipata wasiwasi hivi karibu TAA amekuwa anapoteza mipira akiwa pressed vizuri kwenye phase ya kwanza pale wanapokuwa 3-2 ndio maana leo aliamua iwe 4-2 ili phase ya kwanza TAA asiwe kwenye kiungo lakini wakifika phase ya pili maana yake kwenye kiungo basi TAA ndio anakuja ndani kwasababu eneo hilo Villa wanakuwa wachache kwahiyo ngumu kwake kufanyiwa pressing na alikuwa anapata muda na nafasi ya kutosha akiwa na mpira kupiga pasi zake hatari nyuma ya safu ya ulinzi ya Villa
✍🏻Leo ni ile siku ambayo Aston Villa walikuwa kama walivyocheza dhidi ya Newcastle,vitu vingi walifanya chini ya standard inayotakiwa ushahidi nu kumuona kocha wao Unai kwenye benchi jinsi alivyokuwa anatupa mikono kwa hasira
1: Unakabia juu wakati viungo na washambuliaji wako hawaweki presha kwenye mpira ?? Tena dhidi ya wapasia mpira hodari ( TAA na Mac Allister ) ..unatafuta shida hapo
2: Kurudi nyuma kuzuia ( recovery runs ) zao ukiacha Konsa wengine walikuwa wana switch off kiasi kwamba Salah Diaz na Nunez walikuwa wanatafuna tu space nyuma yao 😀
3: Maamuzi wakifika lango la Liverpool yaliwaangusha pale walipotakiwa kuwa na ufanisi
NOTE
1: Liverpool ilikuwa wachague wao tu ni mangapi wafunge , nafasi bora nyingi walitengeneza
2: Szobo . Kila kitu anafanya : kuzuia , kutengeneza , sio mvivu uwanjani . Ameanza maisha yake Anfield vizuri sana
3: Ule utatu wa Liverpool wa leo Diaz Darwin na Salah unatishia amani hasa wakifungua " TURBO " zao 🔥🔥
4: Mpe muda na nafasi kwenye mpira TAA , then subiria adhabu yako . Pasi zake 🔥
5: Douglas Luiz good player
FT: Liverpool 3-0 Aston Villa
0 Comments