Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KOCHA WA SIMBA ATAWEZA KUWAONDOA AL AHLY KWENYE SUPER LEAGUE??

 


🗣️ Baada ya ratiba ya mashindano ya Caf Africa Fotball League kutoka na klabu ya Simba kupangiwa na klabu ya Al Ahly ya misri watu wengi na wadau wa soka Tanzania wemekuwa wakijipa moyo kuwa huenda Simba ikamtoa M’babe wa Africa kutokana na historia ikionyesha Simba ilishapata ushindi mara mbili dhidi ya Al Ahly

🗣️Mwaka 2019 Simba ilipata ushindi dhidi ya Al Alhy wa bao moja kwa bila chini ya kocha Patrick Ausems goli likifungwa na Madie Kagere kwenye hatua ya Makundi, huku mechi ya kwanza ugenini Simba ilifungwa bao tano dhidi ya Al Ahly, Simaba pia ilipata ushindi Chini ya kocha Didier Gomes Da Rosa bao likifungwa na Jose Luis Miquissone zote zilikuwa mechi za hatua ya Makundi, Simba haijwahi wala kukutana na klabu ya Al Alhy kwenye hatua ya mtoano na hii ni mara ya kwanza Simba anaenda kupata testi mpya au jua kali ya Al Ahly katika hatua ya mtoano

🗣️Mpaka sasa Kocha Robertinho hajaweza kuitengeneza Simba kucheza kwenye ubora wa kitimu zaidi kwa sasa Simba inategemea ubora mchezaji kushinda mechi, Kipindi cha nyuma wakati Simba inapata matokeo mazuri nyumbani dhidi ya Al Alhy katika vipindi tofauti na makocha kama Patrick Ausems na Didier Gomes hakuna anaebiasha Simba ilikuwa bora kitimu zaidi kuliko kutegemea ubora wa mchezaji pekee kuamua matokeo, Hivyo chini ya kocha Robertinho ni ngumu Simba kupenya kuingia hatua ya nusu fainali, Pia kocha huyo ana mifumo ya kizamani na hataki kubadilika kuendana na kasi ya soka la kisasa



Post a Comment

0 Comments