🗣️Mawinga wengi duniani wanaweza kucheza sana eneo la pembeni mwa uwanj yani kulia na kushoto, Hata wakibadilishiwa majukumu na kucheza katika maeneo mengine yani eneo la kiungo wa kati au eneo la mshambuliaji wa kati bado hushindwa kuonyesha ubora kama anavyokuwa katika eneo lake hasilia
Mpaka sasa ndani ya klabu ya Yanga Max Nzengeli tayari amesha pangwa ndani ya uwanja kwenye maeneo matatu tofauti
1) Amepangwa kama winga asilia yani upande wa kulia na upande wa kushoto, Ameonyesha utofauti kati ya winga wa kawaida na winga mbunifu kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira, Uwezo wa kupiga pasi za chini na juu, Uwezo wa kukimbia juu na chini kumsaidia beki wake wa pembeni kuzuia mashambulizi
2) Amepangwa nyuma ya mshambuliaji wa kati yana namba 10, Max pia ameonyesha uwezo wake wa kufunga mabao ya aina yote, Ameonyesha pia uwazo wa kuingia kwenye nafasi ya kuminane ya mpinzani kuongeza namba ya washambuliaji na kusumbua ngome za wapinzani
3) Amepangwa eneo la kiungo wa kati kwenye viungo watatu, Ameonyesha uwezo wake wa kuichezesha timu na kuunganisha eneo la kiungo na eneo la ulinzi, Ameonyesha uwezo wake wa kukimbia eneo kubwa la uwanja akitokea eneo kiungo kiufundi tunawaita ( Box to Box Midfielder) anakuwa na faida kwenye kukaba, Anakuwa na faida kwenye kushambulia na kuitengeneza timu uwiano stahiki kwenye mchezo
0 Comments