Miongoni mwa vitu vilivyonihamasisha kuja Yanga ni pamoja na kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika , nafikiri ni mashindano bora kwenye bara hili lakini pia nafikiri imepita miaka 25 tangu klabu hii icheze hatua ya makundi ya mashindano haya.
Kesho ni mchezo mwingine mpya, tutacheza bila kufikiria matokeo ya Kigali, Rwanda, tutacheza kama matokeo ni 0-0. Tumefanya kazi kwa bidii na tunasubiri kesho kuonesha mchezo mzuri na kuwapa furaha wananchi.
- Miguel Gamondi, Kocha Mkuu Yanga.
0 Comments