Hot Posts

6/recent/ticker-posts

ALICHOKISEMA MWAKINYO REDIONI LEO KABLA YA KUPANDA ULINGONI


Kuna changamoto kati yangu na promotion ambayo nafanyanayo kazi, kwanza niliwafatilia baada ya kuwa wametaka kufanya kazi na mimi na nikakuta kuna baadhi ya tuhuma kwa mabondia waliowahi kufanyanao kazi kuwa hawakulipwa na wanawazungusha.

Nikaona labda ni hila tu za mabondia wa nyumbani kwamba wakati mwingine wanataka event ikiisha basi mtu alipwe chake palepale, kwa hiyo sikuchukulia kwa uzito mkubwa. 

Aliyenikutanisha na Mkurugenzi wa hiyo promotion ni mtu ambaye ninamuheshimu sana kwa hiyo niliwaheshimu kwa heshima ambayo ninayo kwa huyo mtu.

Moja ya makubaliano yetu ni kufanya kazi kama promotion mbili na sio kama bondia, kila mmoja alikuwa na haki kuleta mdhamini au kuleta jambo mezani kujadili na sio kwakuwa wao ni promotion basi wataamua kila jambo na watakalosema ndio liwe. 

Maana ya kuwa na promotions mbili ilikuwa pia mimi niwe na haki ya kuleta mabondia wangu ambao nawaandaa ili nao wapate nafasi ya kupigana kwenye hilo pambano ambalo na mimi nashiriki.

- Hassan Mwakinyo | LeoTena @cloudsfmtz

 

Post a Comment

0 Comments