Timu ya Taifa ya Burundi jana usiku imeshindwa kufuzu Fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast baada ya kupoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Cameroon ambao ulikuwa unaamua hatma ya timu zote mbili kufuzu au kutofuzu!
Ilikuwa ni mechi muhimu kwa Burundi na Cameroon, Burundi ikihitaji ushindi ili kufuzu AFCON 2023 wakati Cameroon yenyewe ilihitaji ushindi au sare ili kufuzu AFCON 2023!
Kundi C lilikuwa na timu tatu tu [Cameroon, Namibia na Burundi] kwa sababu Kenye iliondolewa kwenye huu mchakato baada ya kufungiwa.
Kabla ya mechi ya jana usiku, Namibia ilikuwa kinara wa kundi hilo ikiwa na alama tano [5] Cameroon na Burundi kila moja ilikuwa na alama nne [4].
Baada ya Cameroon kushinda dhidi ya Burundi imemaliza ikiwa kinara wa Kundi C ikifatiwa na Namibi ambazo kwa pamoja zimefuzu AFCON 2023 na kuiacha Burundi.
FT| 🇨🇲 CAMEROON 3-0 BURUNDI 🇧🇮
⚽️ Bryan Mbeumo
⚽️ Christopher Wooh
⚽️ Vaboubakar Vincent
0 Comments