Kipa Beno Kakolanya ambaye alikaa golini kwenye mechi ya ugenini ya Tanzania dhidi ya Algeria Alhamisi iliyopita, amesema wenyeji Algeria walipofanya mabadiliko na kumuingiza staa wa zamani wa Man City Riyad Mahrez,hakuingia hofu na hakutaka kuanza kufikiria ukubwa jina lake kwani angeanza kukaribisha mashambulizi.
“Ipo hivi,ningeanza kufikiria ukubwa wa jina lake,rekodi zake ningekaribisha mashambulizi ya kufungwa golini.
Kichwani mwangu kulijaa kuzuia timu isifungwe muda wote niliokuwepo uwanjani,” —Amesema Beno Kakolanya kupitia gazeti la Championi
“Baada ya mchezo ndio akili inakuja tumecheza na staa mkubwa,hilo halina ubishi kwani CV ya Jamaa ipo wazi na ni ndoto ya kila mchezaji kufika mbali” alisema kipa huyo ambaye aliiongoza Tanzania kupata pointi moja kwenye mechi hiyo na kufanikiwa kufuzu michuano ya AFCON 2023
0 Comments