Hot Posts

6/recent/ticker-posts

ALGERIA WANAZIOGOPA SANA TIMU ZA TANZANIA KWA SASA


Nilipokuwa Algeria kwa ajili ya mechi ya Algeria vs Tanzania, niliwauliza mashabiki kadhaa kuhusiana na ushiriki wa klabu zetu kwenye mashindano ya CAF [Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho].


Msimu uliopita Yanga ilicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya USM Alger ya Algeria, Simba ilicheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.


Waliniambia kuwa, klabu za Algeria hazitamani tena kukutana na klabu za Tanzania, lakini zamani walikuwa hadi wanatengeneza mazingira ya kupangwa na klabu za Tanzania.


Sasa hivi klabu za Tanzania zimekuwa sio salama tena kwao kuja kupita na kwenda hatua inayofata!


- Alex Luambano | #HiliGame cloudsfmtz
 

Post a Comment

0 Comments