Wapinzani wa Simba SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Power dynamos wameshinda mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya Nkwazi FC kwa mabao 2-1 kati ya michezo mitatu waliyocheza na kutoka suluhu katika michezo miwili dhidi ya Prison Leopards na Konkola Blades.
Katika mchezo huo dhidi ya Nkwazi FC mabao yalifungwa na wachezaji Owen Tambo na Joshua Mutali ambaye kocha wa Simba Robertihno amemtazama kama mchezaji hatari zaidi katika kikosi Cha wapinzani wake.
Katika michezo mitatu ya ligi waliyocheza Power dynamos wamefanikiwa kufunga mabao mawili tu na kuruhusu bao moja huku wapinzani wao Simba katika michezo miwili ya ligi wamefunga mabao sita na kuruhusu mabao mawili tu katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar
Tangu Agosti 20, Simba hawajacheza mchezo wowote wa kimashindano licha ya kucheza michezo mitatu ya kirafiki waliyocheza dhidi ya Cosmopolitan, Ngome na Kipanga FC na kufunga mabao 14 kwa ujumla na kuruhusu bao moja tu
Tangu Agosti 19 Power Dynamo wao wamecheza michezo mitano ya kimashindano ligi kuu pamoja na ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wameweza kufunga mabao manne kwa ujumla na kuruhusu mabao matatu.
0 Comments