Hot Posts

6/recent/ticker-posts

USIYOYAJUA KUHUSU CARLOS TEVEZ NA DILI LAKE LA KWENDA CHINDA KUCHEZA KABUMBU


 Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Manchester City, Juventus na timu ya taifa ya Argentina, Carlos Tevez amesema watu wengi walimkosoa pale alipoamua kwenda kucheza soka nchini China.


“Watu wengi walinikosoa sana kwa sababu niliamua kwenda China. Lakini kiuhalisia hawajui historia yangu.”


“Baada ya lile ‘dili’ la uhamisho kukamilika, nilipata kiasi kikubwa cha pesa. Unajua nilifanya nini? Nilimwambia wakala wangu kwamba, sihitaji kiasi chochote cha pesa, nilihitaji kununua nyumba 15 na kuiondoa familia yangu kwenye makazi ya Fuerte Apache.”


“Hakuna hata mtu mmoja aliyefahamu juu ya hilo, lakini najitahidi kusaidia familia 15 ikiwa ni pamoja na kaka zangu, wajomba n.k. Kama utaamua kuhesabu basi ni zaidi ya watu 60.”


“Kila nilichofanya ilikuwa kwa sababu nilitaka kizazi kipya cha Tevez kuwa na maisha bora, kupata elimu bora na sio kupitia maisha niliyopitia mimi.”

Post a Comment

0 Comments