Msimu wa Pili wa mashindano ya Dodoma Ndondo Cup 2023 umezinduliwa rasmi leo Jijini Dodoma na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari za Michezo Jijini Dodoma.
Mh. Mavunde amesema mashindano hayo yana lengo la kutengeneza jukwaa la wachezaji wa Dodoma kutambulika kimkoa na kitaifa na kuendeleza vipaji vyao vitakavyowasidia kuwapatia Ajira kupitia tasnia ya michezo.
Zawadi za Mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa kwa pamoja na Clouds Media Group Mh. Anthony Mavunde na kampuni ya Haier
-Bingwa
Tsh 10,000,000 Kombe na Medali
-Mshindi wa Pili
Tsh 5,000,000 na medali
-Kikundi Bora cha Ushangiliaji
Tsh 1,000,000
-Mfungaji Bora,Kipa Bora na Mchezaji Bora
Tsh 500,000 kwa kila mmoja
Akitoa maelezo ya awali,Mratibu wa Ndondo Cup Ndg. Yahaya Mohamed “Mkazuzu” amesema jumla ya Timu 32 zinatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo usajili wake utafungwa Tarehe 01.09.2023
Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dodoma(DOREFA) Ndg. Mweri Hamsini amesema ligi hiyi inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 10.09.2023 na itafanyika katika viwanja vya Shell Complex-Chamwino,Shule ya Msingi Chang’ombe na Mtekelezo(Central Secondary).
0 Comments