Huko Simba mambo bado, juu ya ile inshu ya mabadiliko ya klabu hiyo ili iendeshwe kwa mfumo wa hisa ambao mchakato wake ulianza tangu mwaka 2017 umekwama ikielezwa tatizo likiwa ni Katiba ya Klabu hiyo, kiasi cha Ofisi ya Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kurudisha mpira Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Simba inapambana kutaka klabu hiyo iendeshwe kisasa kwa hisa na tayari imekuwa ikimtangaza Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed 'Mo' Dewji kuwa ni mwekezaji wake akidaiwa kumiliki asilimia 49 ya hisa, huku 51 zilizobakia zikiwa ni za klabu.
Mchakato unaelezwa ulishapata ruksa kwa Tume ya Ushindani nchini (FCC) kisha Ofisi ya Wakala na Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na sasa ilitua RITA ambako maofisa wake walijifungia kufanya uchambuzi wa kina na kubaini kuna tatizo katika Katiba ya Klabu hiyo.
Source Gazeti la Mwanaspoti
0 Comments