Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC KUONDOKA NA MASHABIKI KWENDA ZAMBIA

"Tumerejea mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo unaofata dhidi ya Power Dynamos. Wachezaji wote wamerejea isipokuwa golikipa Ayoub kutoka Morocco ambaye anarejea leo na moja kwa moja atajiunga na wenzake."


"Tuna siku nyingi za kufanya mazoezi na hivyo menejimenti inaangalia namna gani kikosi kitaweka kambi ya kujiandaa. Mazungumzo yamejikita katika sehemu mbili, moja kuweka kambi kwenye nchi za jirani au tuweke kambi ndani ya Tanzania katika maeneo mengine."


"Katika kipindi chote cha kambi tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki. Tunasubiri uthibitisho wa timu ambazo tutacheza nazo, moja ya nje na nyingine ya ndani. Lengo letu kama Simba ni tupate mechi ngumu, mechi ya kiushindani."


"Taarifa njema ni kwamba Aubin Kramo na Henock Inonga wamepona na wamerejea mazoezini na wenzao."


"Kuelekea mechi yetu dhidi ya Power Dynamos tunategemea kupeleka mashabiki kama ilivyo kawaida yetu tunapokuwa na mechi kwenye nchi za jirani tunatumia basi kupeleka mashabiki, Bahati nzuri Zambia tumeshawahi kwenda huko. Tulipokea maoni tutumie treni na tukafanya mazungumzo na wakawa tayari kutupa punguzo maalumu lakini ratiba za safari ya treni zinapishana na mechi yetu,"


"Utaratibu ambao umeandaliwa na Simba ni tutatoa basi hadi Ndola, Zambia na litarejea nchini baada ya mechi."


"Basi litaondoka nchini kwenda Zambia tarehe 13, Septemba saa 1 usiku na tutafika Ndola, Zambia tarehe 15, Septemba. Tarehe 17, Septemba baada ya mechi basi litaanza safari kurudi Tanzania. Kwa yeyote ambaye anataka kuungana nasi afike ofisini. Kwa kila mtu gharama ni Tsh. 200,000 na anatakiwa kuwa na pasi ya kusafiria na kadi ya manjano. Mwisho wa kupokea nauli ni tarehe 10, Septemba."


Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments