Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA IMEPEWA MPINZANI MGUMU AFRICAN SUPER LEAGUE?


Zikishachekechwa na kubaki timu nane bora Afrika, usitegemee utakutana na mpinzani mwepesi. Kila mpinzani atakuwa mgumu lakini kuna wapinzani wale ambao hutaki kukutana nao kama Al Ahly, Mamelodi na Wydad.


Kwa Simba ni heshima kupata nafasi ya kucheza na kigogo wa Afrika tena kwenye mechi ya ufunguzi wa mashindano, kama Simba ingekuwa inacheza na Enyimba usingekuwa mchezo wa ufunguzi.


Simba vs Al Ahly imepewa hadhi ya kuwa mechi ya ufunguzi kwa sababu ya aina ya timu zinazocheza, Simba kwa Afrika inapata heshima hiyo japo kwa msimu huu inaonekana kama inahangaika kurejesha kile ambacho ilikuwa inakifanya kwa miaka mingi.


- Amri Kiemba | HiliGame @cloudsfmtz
 

Post a Comment

0 Comments