Hot Posts

6/recent/ticker-posts

NYAKATI ZA NEEMA NDANI YA OLD TRAFFORD



✍️ Ni zile nyakati ambazo ukiona fixture ijayo upo na Manchester United unatanguliza maombi mbele kabla ya kwenda kuangalia mchezo wenyewe. 
Siku ya mechi unaomba angalau usifungwe magoli machache. Ukimuona Ferguson unamuona kama mkuu wa kikosi cha maangamizi hivi kumbe ni mwalimu wa mpira.

✍️ Ukiachana na uimara wa safu zao za kiungo pamoja na ushambuliaji, Manchester United walikuwa na ukuta wa chuma bwana. Na leo nimeukumbuka sana ule ukuta wao.
Watu wao kwenye safu ya ulinzi walikuwa na roho mbaya halafu wanaujua mpira sana.

✍️ Nyanda la Kiholanzi EDWIN VAN DER SAR. Piga juu, chini au kutana nae uso kwa uso ilikuwa ngumu sana kumfunga. Yaani hapa hata mabeki walikuwa wanajiamini kuwa mlinda mlango yupo wa kueleweka.
Mbele yake NEMANJA VIDIC na RIO FERDINAND 🙌. Hii pacha haihitaji hata kusimuliwa. Unakabwa kwa kutumia kila kitu ili tu mpira usimfikie Van der Sar.

✍️ Huku mashavuni kuna PATRICE EVRA, upande mwingine weka ASHLEY YOUNG aliyebadilishwa kutoka winga mpaka mlinzi wa kulia. Kama unaona shida weka kijana kutoka Brazil RAPHAEL DA SILVA mwenye roho mbaya.

Na haya yote yanatokea wakati kina CARRICK, JI SUNG PARK na SCHOLES wameshakupunguza nguvu katikati.

Trip ndani ya Old Trafford ilikuwa ndefu na ngumu aisee

✍️ @mlelwa_fred

 

Post a Comment

0 Comments