Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Uraia Pacha Au Kuendeleza Vizazi Vya Mpira? Mjadala Baada ya Kufuzu Afcon 2024


Anaandika wakili wa Timu ya Wananchi "Baada ya timu yetu ya taifa kufuzu michuano ya Afcon 2024, kumekua na mijadala mbali mbali juu ya wachezaji wenye asili ya kitanzania waliobadilisha uraia kutafutwa ili waipambanie nchi.


Japo ni hoja nzuri, mimi nimekua na mtazamo tofauti.


Yaani watu wapambane kivyao na wafanikiwe bila msaada wowote, then tuanze kuhangaika kuwaomba waje wachezee Taifa stars!? 


Kwangu hii sio sawa, ifike mahali watanzania tujenge desturi ya kuvuna tulichokipanda sio kupenda njia za mkato.


Viongozi wetu wakiamua kuzinduka usingizini, wanauwezo mkubwa wa kutengeneza kizazi cha wachezaji wenye uwezo wa kutupeleka mbali kwenye mafanikio ya kisoka, ni vile tu hatupendi kujifunza mambo mazuri kwa waliotuzidi.


Tuwaache vijana walioamua kutafuta maisha sehemu nyingine waendelee kufurahia matunda ya juhudi zao, tusiwasumbue.


Tutengeneze wachezaji wetu, na tusiwakatishe tamaa wanajeshi wetu waliopambana mpaka tukafuzu Afcon ya mwaka 2024.


Uraia pacha sio suluhisho la matatizo yetu kwenye mpira, hakuna mchezaji mzuri atakayepata namba kwenye timu ya taifa kubwa akaacha fursa hiyo akaja kuichezea Tanzania.


#The seeds you plant today, are the fruits you’ll reap tomorrow."
 

Post a Comment

0 Comments